Tuesday, October 16, 2012

Mawaziri na usongo wa kuingia ikulu, sasa kazi zeroSIKU  chache baada ya Raia Jakaya Mrisho KIkwete kuingia madarakani, mwaka 2005, alipata fursa ya kunukuliwa na vyombo kadhaa vya habari vya ndani na nje, kuhusu namna anavyojipanga kuendesha serikali na anataka kuwafikisha wapi Watanzania.
Katika vyombo hivyo, Kikwete alizungumza mengi na hasa matarajio ya serikali yake kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anakuwa na maisha bora. Akaeleza maana pana ya kauli mbiu ya uongozi wake – Maisha Bora kwa Kila Mtanzania na njia za kufika huko.
Sifahamu kama maisha hayo yamepatikana kwa kila Mtanzania kwa kiasi gani, lakini uhakika ni kwamba matarajio makubwa ya rais wetu yamekwama na hakuna njia za kuyahuisha, angalau kwa sasa na kwa muda mfupi wa uongozi wake uliobaki, yakawawezesha Watanzania, kila mmoja wao, kuwa na maisha aliyoyatarajia.
Sababu za hali hiyo ni nyingi, na sijamsikia akizisema, au hata wasaidizi wake wakieleza wazi juu ya mkwamo wa mafanikio ya kauli mbiu hiyo iliyokuwa ikizungumzwa sana miaka kadhaa iliyopita, ingawa sasa imekoma, haipigiwi mbinja zaidi.
Lengo la makala haya mafupi siyo kuchanganua kushindwa ama kufaulu kwa kauli hiyo na uongozi wa Kikwete- la hasha, lakini nimeona vyema tu kuigusia ili kuweka mtiririko mzuri wa hiki ninachokusudia kukieleza; juu ya kuingia madarakani kwa Rais Kikwete na mbio za sasa za baadhi ya viongozi wa juu wa serikali kupigana vikumbo kumrithi hapo muda utakapofika. Muda wa Kikwete kuondoka Ikulu kikatiba ni mwaka 2015.
Nakumbuka moja ya maelezo ya Kikwete aliponukuliwa na vyombo hivyo vya habari ni muda alioutumia ‘kupambana’ kuhakikisha anaukwaa uongozi wa juu wa Tanzania.
“Nimeupigania urais kwa miaka 10, kumalizika tu kwa uchaguzi wa mwaka 1995, ambapo kura hazikutosha, nikaanza mbio hizo kwa kushirikiana na marafiki zangu,” nukuu isiyo rasmi ya Kikwete mwenyewe.
Hiyo ni kauli ya Kikwete, hata kama haitakuwa katika mpangilio, lakini alichokizungumza kinabeba maana hiyo hiyo na hakika kauli hiyo ilionesha namna alivyojipanga kuingia Ikulu pamoja na marafiki zake na watu wengine wa karibu.
Kikwete alitumia miaka 10 kuusaka urais, wenzake, hasa wasaidizi aliowachagua- wengi wakiwa mawaziri, huenda walianza miaka 10 iliyopita, mara baada a yeye  kuapishwa. Na wengine walianza baadaye kidogo, huku wengine wakisubiri kuoteshwa ili waanze mbio hizo za kuingia Ikulu, lakini ieleweke tu kuwa minyukano imekuwa ikishika kasi, tena kubwa kadri siku zinavyokwenda.
Ninachokiona sasa, idadi kubwa ya hao mawaziri, wameshindwa kuwatumikia wananchi. Hawakai maeneo yao ya kazi. Wamekalia siasa. Wamekalia vikao vya mara kwa mara na marafiki zao na watu wengine wa karibu kuunda timu za ushindi.
Watanzania wameshindwa kuona ubunifu wa viongozi wao katika kuwatumikia. Haieleweki kama wameshindwa au wengi wamezoea mkuu aseme – awaongoze kwa kila kitu kata katika maeneo waliyobobea! Inashangaza kuona waziri tangu aingie kwenye nafasi yake hajawahi kufanya jambo la maana na hiyo inaonesha namna wanavyomuangusha hata aliyewachagua.
Au labda wanashindwa ‘ku-deliver’ kwa kuwa mkuu wao anawagomea au wanadhani hatapendezwa na kile watakachoamua? Kwa kifupi haieleweki.
Lakini, angalau linaloeleweka ni kwamba wengi wako bize na kutengeneza mitandao yao ya kuwaingiza Ikulu, ili wakale, na ni wachache sana, miongoni mwa hao wanaoutafuta urais kwa udi na uvumba , wana dhamira ya kweli ya kuwatumikia Watanzania zaidi ya kuwa wachumia tumbo tu kama wengine ambao tumewashuhudia.
Nadhani, ingekuwa  vyema sana wanaohangaikia urais wakaacha mara moja na kujikita zaidi kuwatumikia Watanzania kwa nafasi zao za sasa na kama wanaonekana wanafaa, chama chao kitawaweka juu ili kugombea nafasi ya kuingia Ikulu.
Wakati umefika sasa, kwa vyama vya siasa kuona umuhimu wa kuwa na utaratibu wa kuwapa nafasi wanachama wao kugombea urais kutokana na uchapakazi wao, uzalendo wao, uwezo wao, utayari wao na mengine mazuri yanayofanana na hayo na kuwakataa kabisa wooote wanaounda makundi ya kuwaingiza Ikulu.
Madhara ya viongozi kuunda mitandao ya mbeleko za kuwaingiza Ikulu tumeyaona na ni vyema sasa kuwakana hao wachumia tumbo, ili mwisho wa siku apatikane anayefaa na tusiwe na shaka na utendaji wake.
Tafakari.
Mungu ibariki Tanzania.

1 comment:

Anonymous said...

Just as the gods used WWII to justify an influx of new technologies, including the voice in your head, so will they use the impending pestilence which kills over half the world's population to justify historical medical advances, including the "cure of aging", initiating the "1000 years with Jesus on Earth", despite biotechnology already accomplishing these goals.
We've seen this tactic used recently with AIDS, targetted at homosexuals and blacks in Africa with the biotechnology product. The gods control everything on Earth, and althugh sold AIDS to your enemies as revenge, their real purpose was to enlighten you regarding sex:::Back-handed help. It was very effective with homosexuals in the USA, but sex is among the most powerful temptations with Africans. Remeber it is always the gods:::Slavery, AIDS, drive-bys, crack babies, pimps prostituting 10 year-old girls. And, contrary to your belief the victim doesn't go anywhere, they are reincarnated back to Earth like everyone else when we die.
Then, as promised, The End will come with fire::::Global tectonic subduction.

There was a very real perception that bi-racial was much worse for the white than it was for the person of color. The liberal culture, which was designed and promoted with the god's tools to achieve their Apocalyptic goals, screamed racism when there was a very reasonable explanation for this reality::::
In this white punishment known as the United States the person of color has already adopted the disfavors/temptations intended for another race. But by associating/mating with a person of color the white is newly adopting the disfavors of another culture.
And this is the reason why people of color are not welcome in the United States. The gods control everything:::The perception they want to create, the thoughts they want you to have.
People of color can't recover from absorbing the temptations from two cultures. And why they become more and more like so many blacks in America:::Veterans at absorbing the temptations of two cultures.
To further illustrate this is why California's educational system/funding was ranked #1 when California was white:::Education being the basis of the affluent economic system. Now even public higher education has become unaffordable.

Don't forget the lessons the 'ole white preacher taught:::Dancing is a sin, spare the rod spoil the child.
The gods used the liberal tool to ridicule away so many taboos, paving the way for the decay of society and ultimately the End Times::::::
Black behavior was controlled by the KKK. Men's behavior was controlled by marriage for thousands of years.
When married by 15 men never gained the taste of promiscuity. Once the gods used the budding liberalism tool the men set the tone for the deteriorating enviornment centered around their gross disfavor.
Women's relinquishing control of pre-arranged marriage will be what costs mankind everything in The End. It's all their fault. Men are pigs, essentially just primally responsive disfavored beings who if given the freedom will abuse based on the impulses the god's push them into. Whereas under pre-arranged marriage this behavior was contained now the promiscuous fraternity house epitomizes the pinnicle of what a "real man" should be like. And sadly the women fall into line.

The gods behave monsterously in the course of managing Planet Earth but they demand people be good if you are to have a chance to ascend in a future life.
Not only is doing the right things important (praying, attoning for your sins, thinking the right way:::accepting humility, modesty, vulnerability), so is avoiding the wrong things important as well:::"Go and sin no more".
You NEED active parents who share wisdom to have a real chance to ascend into heaven in a future life, and you MUST be a good parent as well to have that opportunity. Once your children have been raised something changes, something has been decided about you. This is exactly that.